ANGALIA PICHA_CHADEMA WAFANYA MKUTANO MKUBWA SHINYANGA MJINI- LWAKATARE AUNGURUMA,VIONGOZI WAPYA WATAMBULISHWA

Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako jioni ya leo kumefanyika mkutano mkubwa wa CHADEMA uliolenga kutambulisha viongozi wapya wa Chama hicho katika wilaya ambao wamechaguliwa mapema mwezi huu,mgeni rasmi alikuwa  Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare.Pichani ni viongozi mbalimbali wa Chadema ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga waliohudhuria mkutano huo..Orodha ya viongozi wapya iko mwishoni mwa picha zote hapo chini-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Kushoto ni katibu mpya wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini Mussa Ngasa maarufu kwa jina la Goma la Manzese ama "Machimu Kenda" (mikuki 9) akiwasalimia wakazi wa Shinyanga mjini ambapo alisema CHADEMA imejipanga vyema katika kuhakikisha inachukua uongozi kuanzia ngazi ya chini hadi juu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Kushoto ni mwenyekiti mpya wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini ndugu Hassan Baruti akimkabidhi kadi ya CHADEMA bi  Damari Nyantabano aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Mapya kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga kupitia CCM ambaye ameamua kuhamia Chadema kwa madai kuwa CCM imejaa ukiritimba.Mwanachama huyo mpya wa CHADEMA alikabidhi kadi zake zote za CCM na kupokea kadi ya CHADEMA-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bi  Damari Nyantabano aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Mapya kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga kupitia CCM akishikana mkono wa karibu Chadema kutoka kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ndugu Juma Protas naye alikuwepo,hapa anawasalimia wakazi wa Shinyanga mjini na kuongeza kuwa yupo tayari kufanya kazi na timu mpya wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akizungumza na wakazi wa Shinyanga jioni ya leo ambapo aliwataka  watanzania kubadilika kwani CCM imeshindwa kuwaleta maisha bora kwa miaka zaidi ya 50 sasa,kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu.Alisema uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao wasifanye makosa kuipa kura CCM bali waipe Chadema kwani ndiyo mkombozi wao-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 
Waandishi wa habari wakifanya yao wakati wa mkutano wa Chadema jioni ya leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa Chadema jioni ya leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akionesha rasimu ya katiba mpya ambayo alidai CCM hawaitaki kwa sababu inawabana na kuwafanya waendelee kuwa,wezi mafisadi na kutumia rasilimali za taifa kwa maslahi yao binafsi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527