YULE KIJANA KINARA WA KUBAKA,KULAWITI NA KUTOBOA MACHO WATOTO SHINYANGA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI

Kushoto ni kijana aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka,kulawiti na kutoboa macho watoto


Kulia ni Jacob Mayani kinara wa ubakaji,ulawiti na kutoboa macho watoto Shinyanga

Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kesi tatu tofauti.

Mtuhumiwa huyo Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha kwenye MAHAKAMA ya  Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.

Jacob Mayani ambaye alituhumiwa kuhusika na  matukio tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya miaka 10 sanjari na kuwatoboa macho amejikuta akiishia gerezani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527