Maajabu Haya!! TAZAMA PICHA KIJANA HUYU ANG'OLEWA MENO 232,YABAKI 28,ALIKUWA NA MENO 260


Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba.

Kijana huyo Ashik Gavai

Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.

Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo.

Meno yaliyong'olewa

Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia".
Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili. 

Ashik sasa ana meno 28,alikuwa nayo 260.

"Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. 

Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware.

"Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.

"Tulivyopasua tu, meno madogo madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na tulipoyahesabu, yalifika meno 232." Amesema daktari huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527