HII HAPA NDIYO RATIBA YA SWALA YA SIKUKUU YA IDD EL FITRI


Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao maalumu katika Ofisi za  Mkoa wa Dar es Salaam za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) jana, Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo sambamba na hotuba mbalimbali inatarajiwa kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo inatarajiwa kuwa siku ya Jumatatu Julai 28 au Jumanne  Julai 29 mwaka huu.
 

Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa Kiislamu na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika saa 9 Alasiri katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni Rasmi wa Baraza hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527