DIAMOND ATWAA TUZO ZAAFRIMMA NCHINI MAREKANI


STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametwaa tuzo moja ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki katika Tuzo za Afrimma zilizofanyika Dallas. TX nchini Marekani.


Tuzo zilifanyiwa kwenye jengo hili
Zinaitwa African Muzic Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.

Good news kwa mujibu wa meneja Babu Tale ni kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’ Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.

Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.

Producer bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.

Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527