Bad News_ALIYEKUWA MHADHIRI MWANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM-SJMC) DR KAPOLI AMEFARIKI DUNIA


Dr. Irenius Kapoli enzi za uhai wake

Habari zilizoufikia mtandao huu wa malunde1 blog zinasema kuwa aliyekuwa mhadhiri mwandamizi katika chuo kikuu cha Dar es salaam(Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma-SJMC) Dr Ireneus Kapoli amefariki dunia leo (Jumamosi)alfajiri.

Chanzo chetu cha habari kimeiambia malunde1 blog kuwa Dr Kapoli amefariki dunia 
katika hospitali ya Tumbi
 huko Kibaha kutokana na BP na Kisukari. 

 Alikimbizwa hospitalini baada ya kuugua ghafla.  

Taarifa zinasema kuwa msiba uko nyumbani kwake Mbezi (Malamba mawili) jijini Dar es salaam na mazishi yanatarajia kufanyika kesho kutwa 
siku ya Jumatatu hapo nyumbani kwake.

Dr Kapoli alikuwa mtaalam wa lugha ya Kiingereza na alifanya PHD yake nchini Uingereza ,alianza kufundisha Main Campus Mlimani baadaye kuajiriwa katika Shule Kuu ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma(sjmc).


 Alifundisha kwa muda wa zaidi ya miaka 10 hapo UDSM-SJMC,akiwa katika idara ya Lugha na  alistaafu rasmi mwaka jana.

Mbali na kufundisha smjc Dr Kapoli aliwahi kufanya kazi maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kozi alizopata kuzifundisha katika chuo hicho enzi za uhai wake ni "Communications Skills( English for Journalists/Media),"Critical Discourse Analysis" na "Critical Thinking and Argumentation"

Dr Kapoli alikuwa mtanashati,mpenda haki,mshauri mzuri,
mwalimu bora, mwenye msimamo hakupenda upumbavu hata kidogo,,hakika aliyefundishwa na mwalimu huyu atakumbuka mengi mema ya Dr Kapoli.


Hata mkurugenzi wa blog hii ya Malunde1 ndugu Kadama Malunde alifundishwa na Dr Kapoli wakati akiwa mwanafunzi katika chuo hicho mwaka 2008/2011.

Zifuatazo  ni baadhi ya status zilizopostiwa facebook,na jinsi wanafamilia wa SJMC walivyopokea msiba huu


Tunashukuru kwa yote.Tunashukuru kwa kupata bahati ya kuwa wanafunzi wako.Tunashukuru kwa kufanya kazi na wewe.Tunashukuru kwa kuwa tunaamini umetimiza wajibu wako kwa weledi mkubwa.Tunashukuru kwa mfano bora wa maisha yako.Tunashukuru..tunashukuru...R.I.P. Dr. Irenius Kapoli.

Photo: Tunashukuru kwa yote.Tunashukuru kwa kupata bahati ya kuwa wanafunzi wako.Tunashukuru kwa kufanya kazi na wewe.Tunashukuru kwa kuwa tunaamini umetimiza wajibu wako kwa weledi mkubwa.Tunashukuru kwa mfano bora wa maisha yako.Tunashukuru..tunashukuru...R.I.P. Dr. Irenius Kapoli.



++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Dr Kapoli... dah hata sijui niseme nini, zaidi ya kuwa mwalimu bora, alikuwa mwenye msimamo hakupenda upumbavu hata kidogo, kama haustahili kitu ni haustahili full stop, yaani hakuwa na kona kona Abraham Tz utakuwa unaelewa vizuri... dah haya baba tangulia ndo njia yetu sote... May U rest in Peace!

Photo: Dr Kapoli... dah hata sijui niseme nini, zaidi ya kuwa mwalimu bora, alikuwa mwenye msimamo hakupenda upumbavu hata kidogo, kama haustahili kitu ni haustahili full stop, yaani hakuwa na kona kona Abraham Tz utakuwa unaelewa vizuri... dah haya baba tangulia ndo njia yetu sote... May U rest in Peace!

Malunde1 blog itaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu msiba huu


Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Dr Kapoli.Amina!


  • Kadama Malunde
  • Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527